Home Uncategorized HAKUNA CHAMA SIMBA HAKUNA USHINDI, AFUNGA MABAO 2-0 POLISI TANZANIA

HAKUNA CHAMA SIMBA HAKUNA USHINDI, AFUNGA MABAO 2-0 POLISI TANZANIA


 CLATOUS Chama, kiungo ndani ya Klabu ya Simba amedhihirisha kwamba yeye ni mchezaji tegemeo ndani ya kikosi hicho kwa kuweza kubadili matokeo baada ya kuingia kipindi cha pili na kufunga mabao 2-0 wakati timu yake ikishinda mbele ya Polisi Tanzania.


Mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Mkapa dakika 45 za kipindi cha kwanza ubao ulikuwa unasoma 0-0 huku timu zote zikiwa zimetoshana nguvu katika mashambulizi na ulinzi.


Kipindi cha pili, Sven Vandenbroeck alifanya mabadiliko kwa kumtoa Bernard Morrison ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama pamoja na John Bocco alingia akichukua nafasi ya Francis Kahata.


Chama amekuwa nyota wa mchezo wa leo kwa kufanya kazi ya ziada ya kubadili ushindi ambapo bao la kwanza alifunga dakika ya 65 kwa pasi ya John Bocco na bao la pili alifunga dakika ya 89 kwa pasi ya Said Ndemla.


Malale Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa Simba imepata ushindi kwa sababu ya Chama kwani asingekuwepo mchezaji huyo walikuwa wameshawadhibiti.


“Tulikuwa tunafanya vizuri mwanzo ndio maana kipindi cha kwanza tuliweza kutoshana nguvu, kipindi cha pili alipoingia Chama hapo ndipo mambo yalibadilika.


“Yeye alicheza mpira anaoujua na hakukuwa na ile tunasema kwamba kuna timu bali ni uwezo wa mchezaji mmoja, hivyo tumeshindwa kwa sababu hatukuwa na mchezaji wa kuamua matokeo,” amesema.


Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 26 ikiwa nafasi ya tatu na Polisi Tanzania inabakiwa na pointi 20 ikiwa nafasi ya sita.

SOMA NA HII  BREAKING: LWANDAMINA ATUA AZAM FC KUCHUKUA MIKOBA YA CIOABA