ABUTWALIB Mshery, kipa namba moja wa Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Badru Mohamed anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga na Simba ambao wapo kwenye mpango wa kuboresha vikosi vyoa kwa sasa.
Kipa huyo amekuwa chaguo la kwanza kwa makocha wote ambao wamepita katika kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo kambini kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za lala salama.
Ilikuwa zama za Zuber Katwila ambaye kwa sasa yupo Ihefu, Hitimana Thiery ambaye alibwaga manyanga na kwa sasa chini ya Mohamed.
Nyota huyo mzawa kwenye mechi zote za Simba na Yanga alikaa langoni jambo ambalo limewafanya mabosi hao kuanza kumfuatilia kwa ukaribu ili kupata saini yake na huenda wakampata bure kwa kuwa kandarasi yake ipo ukingoni.
Anakumbuka kwamba kwenye kichapo cha Simba 5-0 Mtibwa Sugar namna alivyopata tabu na wakati ule ubao ukisoma Yanga 1-0 Mtibwa, licha ya jitihada zake kuokoa hatari ila hakuweza kuipa pointi timu yake.
Kuhusu suala hilo nyota huyo amesema:”Mkataba wangu ndani ya Mtibwa Sugar unamalizika, kuhusu Yanga na Simba bado hawajanifuata ila mimi nitaangalia pale ambapo pana maslahi zaidi ikiwa tutafikia makubaliano basi nitajiunga na timu yoyote,” .