Home Uncategorized BREAKING: LWANDAMINA ATUA AZAM FC KUCHUKUA MIKOBA YA CIOABA

BREAKING: LWANDAMINA ATUA AZAM FC KUCHUKUA MIKOBA YA CIOABA

 


BREAKING: George Lwandamina ambaye alikuwa kocha wa Yanga leo Desemba 2 ametua rasmi kwenye ardhi ya Bongo akitokea Zambia kwa ajili ya kuinoa Azam FC akichukua mikoba ya Aristica Cioaba.


Cioaba ambaye alikuwa ndani ya Azam FC kuanzia mwanzo wa msimu alifutwa kazi Novemba 26 Siku moja baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga Uwanja wa Azam Complex. 

Kwa sasa timu ipo mkoani Mwanza ambapo Desemba 7 itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Gwambina Complex ikiwa chini ya kaimu kocha msaidizi, Vivier Bahati.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Lwandamina amesema kuwa amekuja ndani ya Azam FC kufanya kazi hivyo mashabiki wampe sapoti.

“Nimefurahi kuja tena ndani ya Tanzania, nilikuwepo nikaondoka na sasa nimerudi tena, imani yangu ni kwamba tutakuwa pamoja katika kufikia mafanikio,” amesema.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC,Abdlkarim Amin amesema kuwa wamefanya mchakato wa kumleta baada ya kuukubali uwezo wake na wanaamini atakwenda sawa na sera ya Azam FC.

“Kwa muda tulikuwa tunamfuatilia na tunatambua kwamba analijua soka la Bongo hivyo hatuna mashaka katika hilo, kikubwa mashabiki wawe pamoja nasi kazi bado inaendelea,” amesema.
SOMA NA HII  KUMBE, HAKUKUWA NA MAELEWAMO MAZURI KATI YA KOCHA ALIYEFUTWA KAZI NA MABOSI WA NAMUNGO