Home Uncategorized SAMATTA ATANGAZA KUREJEA SIMBA

SAMATTA ATANGAZA KUREJEA SIMBA


Straika tegemo katika timu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji, Mbwana Samatta, amesema kuwa endapo atamaliza harakati za maisha yake ya soka atarejea Tanzania kuungana na Simba.

“Wachezaji wengi wakubwa wanapokaribia kustaafu soka hurudi kwenye vilabu vyao vya zamani ambavyo viliwatoa.

“Nilikuwa mchezaji wa Simba zamani, hata nitakaporudi baadaye nafikiri nafasi ya kwanza itakuwa kwa Simba kwa sababu niliwahi kuitumikia lakini kama watakuwa hawanitaki ndio nitaangalia sehemu nyingine.
.
“Kwa heshima yao kwa sababu niliwahi kuwa mchezaji wao kwa hiyo nafasi ya kwanza lazima itakuwa kwao.”

SOMA NA HII  SAMATTA ANAAMINI WATANZANIA WOTE WATAMPA SAPOTI