Home Azam FC AZAM FC YATUMA SALAMU SIMBA, MTAMBO WAO WA MABAO KUKOSEKANA

AZAM FC YATUMA SALAMU SIMBA, MTAMBO WAO WA MABAO KUKOSEKANA


 KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa wamejipanga vema kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mechi zao ambazo zimebaki ili kupata ushindi.

Kesho, Azam FC inatarajiwa kuwakaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utapigwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku.

Kwenye mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-2 Azam FC huku nyota wa Simba, Clatous Chama akikumbuka kwamba penalti yake iliokolewa na kipa wa Azam FC Mathias Kigonya.

Ipo nafasi ya tatu Azam FC pointi zake kibindoni ni 64 baada ya kucheza jumla ya mechi 32 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 79 baada ya kucheza mechi 32.

Bahati amesema:”Kwa mechi ambazo zimebaki hatuna namna ambayo tunahitaji kufanya zaidi ya kuona kwamba tunapata ushindi kwani hilo ni jambo la kwanza.

“Kila mchezaji anapenda kuona timu inashinda na kupata pointi tatu hivyo tupo imara na tunajua kwamba tutakutana na timu imara hakuna namna tutapambana ili kupata pointi tatu,” .

Tayari Simba ni mabingwa wanatarajiwa kukabidhiwa taji lao Julai 18, Uwanja wa Mkapa hivyo hawana cha kupoteza zaidi ya kusaka heshima huku Azam FC wakiwa wanapambania malengo yao ya kumaliza ndani ya nafasi ya pili iliyo mikononi mwa Yanga.

Katika mchezo wa kesho, Simba itakosa huduma ya nyota wake Francis Kahata ambaye alikuwa na urafiki mkubwa na Meddie Kagere hasa walipokuwa wakikutana na Azam FC kwa kuwa alikuwa mtambo wa kutengeneza mabao.

Sababu kubwa ya Kahata kukosekana ni kwamba mkataba wake ulimeguka na mabosi wa Simba hawakuwa tayari kumuongezea mkataba.

SOMA NA HII  DUBE: KWA BEKI HUYU, SIMBA WAMEPATA JEMBE