Home Uncategorized MANCHESTER UNITED, CHELSEA KUAMBULIA PATUPU KWA SANCHO

MANCHESTER UNITED, CHELSEA KUAMBULIA PATUPU KWA SANCHO


KLABU ya Borussia Dortmund inayommiliki nyota Jadon Sancho anayehusishwa kujiunga na Manchester United imesema kuwa nyota huyo haondoki.

Dortmund imesisitiza kwa msisitizo kwamba Manchester United, Chelsea na Liverpool zisahau habari ya kumpata nyota huyo kwenye usajili wa majira ya joto Ulaya.

Sebastian Kehl, Mkuu wa Masuala ya leseni ya Klabu ya Borussia Dortmund amesema kuwa nyota huyo msimu ujao atacheza Ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

“Tunatarajia Jadon atacheza kwenye timu yetu msimu ujao, hataondoka kwenda kwingine”.

SOMA NA HII  SAIDO NTIBANZOKIZA KUANZA NA DODOMA JIJI