Home Habari za michezo CHAMA NA SIMBA KWA MSIMU HUU NDIO BASI TENA….TFF WATIBUA KILA KITU…

CHAMA NA SIMBA KWA MSIMU HUU NDIO BASI TENA….TFF WATIBUA KILA KITU…

Habari za SImba SC

NYOTA wa Simba, Clatous Chama amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh 500, 000 kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Ruvu Shooting, Abalkassim Suleiman.

Taarifa liyotolewa leo na Bodi ya Ligi (TPLB) ilieleza tukio hilo lilitokea wakati wachezaji hao wakiwa hawagombei mpira jambo ambalo lilisababisha mwamuzi wa mchezo huo kushindwa kuona.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam Mei 12, mwaka huu na Simba kushinda mabao 3-0, ilisambaa video iliyomuonyesha Chama akifanya tukio hilo la wazi.

Adhabu hiyo ni kutokana na kanuni ya 41:5 (5.2) ya Ligi Kuu Bara kuhusu uthibiti wa wachezaji.

Kutokana na adhabu hiyo, Chama atakosa michezo yote miwili ya kumalizia msimu akianza na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania Juni 6 na Coastal Union Juni 9 ambayo itapigwa jijini Dar es Salaam.

Chama ni miongoni mwa viungo wanaowania tuzo ya kiungo bora wa msimu akishindana na Bruno Gomes (Singida Big Stars), Mzamiru Yassin na Saidi Ntibazonkiza (Simba) na Stephane Aziz KI wa Yanga.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF...WASAUZI WAAMUA KUJA KIMACHALE MACHALE...SIMBA WANASA MIKANDA YAO YOTE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here