Home Uncategorized BEKI HUYU WA SIMBA AWEKWA KWENYE TAGETI ZA YANGA NA AZAM

BEKI HUYU WA SIMBA AWEKWA KWENYE TAGETI ZA YANGA NA AZAM


BEKI wa Simba Juuko Murshid ambaye nafasi yake ya kubaki ndani ya Simba kwa sasa ni finyu imeelezwa kuwa amekuwa ndani ya tageti za Azam FC na Yanga ambao wote ni wa kimataifa.

Habari zimeeleza kwamba tayari uongozi wa Azam FC umeanza kumvutia kasi beki huyo ambaye ndani ya kikosi cha timu ya Taifa Uganda anapeta.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa kwa sasa hawana mpango wa kuzungumza masuala ya usajili wa wachezaji badala yake wamewekeza nguvu kwenye usajili wa kocha ambaye wana mpango wa kumtangaza leo.

SOMA NA HII  YANGA KUMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KMC