Home Habari za michezo MASTAA SIMBA SC WALA KIAPO KUMALIZIA KAZI YA DAR…HISTORIA KURUDIWA..?

MASTAA SIMBA SC WALA KIAPO KUMALIZIA KAZI YA DAR…HISTORIA KURUDIWA..?

ULE MOSHI WAIPONZA WYDAD CAF...WASHTAKIWA NA SIMBA...KUMBE WALIRUKA NA KUINGIA VIP

Wachezaji wa Simba SC wamesema wapo tayari nchini Morocco wakiwa na matumaini makubwa ya kupata ushindi dhidi ya Wydad AC na kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC inatarajiwa kuivaa dhidi ya Wydad AC katika mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali utakaopigwa keshokutwa Ijumaa (Aprili 29), kwenye Uwanja wa Mohammed V, ambao upo mjini Casablanca nchini Morocco.

Katika mchezo huo, Simba SC wataingia uwanjani wakiwa na mtaji wa bao 1-0 waliopata katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza Jumamosi (April 22) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mfungaji wa bao hilo Mkongomani, Jean Baleke amesema kuwa wana nafasi kubwa ya kufuzu Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuitoa Wydad AC.

Baleke amesema kuwa, watakapokuwa Morocco wataingia uwanjani kucheza dhidi ya Wydad AC wakiwa wanawaheshimu kwa kushambulia goli ndani ya wakati mmoja wakijilinda.

“Wachezaji na viongozi tunataka kutimiza malengo yetu ya kufika Nusu Fainali, tunawaheshimu Wydad AC ni miongoni mwa timu bora na ngumu lakini tuko tayari kupambana, jambo zuri ni kuwa tunarudi tena Morocco na mchezo wa mwisho tulicheza dhidi ya Raja Casablanca pale nami nilifunga bao moja,” amesema Baleke

Kwa upande wa Beki wa Kulia Shomari Kapombe amesema kuwa: “Tuna kibarua kigumu katika mchezo wa marudiano dhidi ya Wydad AC, licha ya kupata ushindi nyumbani kwetu.

“Ugumu huo unakuja kutokana na sapoti ya mashabiki wao, tunaamini watajitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuwasapoti, lakini sisi kama wachezaji hatuwaangalii wao na badala yake tutamiza majukumu yetu ya uwanjani,” amesema Kapombe.

Naye Kiungo mshambuliaji kutoka Zambia Clatous Chama amesema: “Walikuwa na bahati kubwa Wydad AC katika mchezo uliopita, kutokana na kupoteza nafasi nyingi za kufunga ambazo tulizipata.”

“Lakini tutarejea nao tena keshokutwa Ijumaa, ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili na sio Simba pekee, kwani licha ya ya wapinzani wetu kuwepo nyumbani, hakutuzii sisi kupata matokeo mazuri, hivyo tunakwenda kufuata ushindi Morocco,” amesema Chama

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA 'KUUPIGA MWINGI' JANA...'TSHABALALA' KAAMUA ISIWE NONGWA..KAIBUKA NA HILI LEO...