Home Habari za michezo KUHUSU KUTINGA NUSU FAINAL CAF….NABI APATA KIGUGUMIZI NA YANGA YAKE…

KUHUSU KUTINGA NUSU FAINAL CAF….NABI APATA KIGUGUMIZI NA YANGA YAKE…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amejikuta akipatwa na kigugumizi juu ya timu anayotamani kukutana nayo kama atafuzu katika hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga SC kwa sasa wapo katika hatua ya Robo Fainali huku mchezo wao wa Mkondo wa Kwanza wakiwa wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ugenini, jambo ambalo ni faida kwao.

Kocha Nabi amesema kuwa: “Sisi binafsi kama Yanga SC bado hatujafuzu kwenda katika hatua ya Nusu Fainali, bado tuna mtihani mbele ya Rivers tukiwa kwetu, kwa wale amabo wanaona kuwa kazi tumemaliza wanatakiwa kutambua huu ni mpira wa miguu.”

“Tunakwenda kuweka mipango yetu kwaajili ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa marudiano, kuhusu nusu fainali siwezi kusema nawataka Marumo wala Pyramid mpaka pale ambapo tutakamilisha ratiba yetu,” amesema kocha huyo.

Yanga SC itakuwa mwenyeji wa Rivers United katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam siku ya Jumapili (April 30) huku ikihitaji ushindi wowote au sare ili kujihakikishia nafasi ya kutinga Nusu Fainali.

Kwa Upande wa Rivers United Itatakiwa kushinda mabao 3-0 au zaidi ili kusonga mbele.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Pyramids na Marumo Gallants kwenye Hatua ya Nusu Fainali.

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA VICHEKO TU KABLA YA KARIAKOO DABI