Home Simba SC UCHAGUZI WA SIMBA NI LEO,SIFA YA MPIGA KURA PIA NI KULIPA ADA

UCHAGUZI WA SIMBA NI LEO,SIFA YA MPIGA KURA PIA NI KULIPA ADA

 


MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba, Boniface Lihamwike amesema kuwa moja ya kigezo cha mwanachama kupiga kura ni kuwa amelipa ada ya uanachama.

Leo, Februari 7, Simba itafanya uchaguzi mdogo wa Mwenyekiti wa Wanachama kuziba nafasi ya Sued Mkwabi aliyebwaga manyanga Septemba, 2019.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar na wagombea wawili ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu.

Lihamwike amesema:-“Moja ya kigezo cha kupiga kura ni mwanachama kulipia ada ya uanachama hivyo nje ya ukumbi wa mkutano kutakuwa na eneo maalumu ambalo watatumia wanachama ambao hawajalipa kufanya malipo.

“Wagombea wawili ambao ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu walikidhi vigezo, hawa ndiyo wanawania nafasi hii ambayo iliachwa na Sued Nkwabi,”.

Mkutano unatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi na kumalizika mapema ili kutoa nafasi ya mashabiki kuhudhuria mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Azam FC.


SOMA NA HII  GOMES - TUNAELEKEZA JUHUDI KWENYE UBINGWA WA LIGI KUU