Home Habari za michezo KUHUSU KUONGEZA MKATABA YANGA…AZIZ KI KAANIKA HAYA MAPYA LEO…

KUHUSU KUONGEZA MKATABA YANGA…AZIZ KI KAANIKA HAYA MAPYA LEO…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga msimu huu imezidi kuwa moto. Inasaka taji la tatu mfululizo la Ligi Kuu Bara. Ndani ya kikosi chake kuna mastaa wa nguvu na wameifanya kugawa vichapo Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika ambako imefuzu hatua ya robo fainali.

Kazi kubwa ya nyota wa timu hiyo chini ya kocha ni kuhakikisha wanafika mbali zaidi. Mmoja wa mastaa hao ni Stephanie Aziz KI, raia wa Burkina Faso.

Ubinifu wa miguu umemtambulisha kuwa kiungo mshambuliaji fundi nchini. Mikwaju ya friikiki, penalti, matobo na chenga za maudhi ni vyake. Utafurahi kumuona. Utatamani achezee timu unayoishabikia ili umfurahie kwenye kila mechi.

Aziz KI yuko kwenye moto msimu huu pengine tangu atue nchini. Ana mabao 11 kwenye Ligi Kuu Bara moja nyuma ya Feisal Salum ‘Feitoto’ anayeongoza kwa ufungaji akiwa na 12.

Kiwango chake kimelilazimisha Gazeti la Mihczo Nchini la Mwanaspoti kumsaka na kufanya naye mahojiano mafupi juu ya jinsi alivyojipanga msimu huu na mambo mengine.

Aziz Ki mkataba wake unafikia ukingoni mwisho wa msimu na hapa anasema hana tatizo la kubaki Yanga na uongozi wa Yanga uko kwenye mazungumzo mazuri na wanaomsimamia.

Mkataba wake unafikia ukingoni mwisho wa msimu na hapa anasema hana tatizo la kubaki Yanga na uongozi wa Yanga uko kwenye mazungumzo mazuri na wanaomsimamia.

“Ni kweli mkataba wangu utafikia mwisho msimu huu, lakini moyo wangu una furaha ya kuwa sehemu ya familia hii ya Yanga. Bado uongozi wangu upo kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga, kila kitu kikimalizika nadhani mambo yatakuwa wazi,“ anasema.

SOMA NA HII  HUYU HAPA MTANZAMIA ALIYENGIA KWENYE REKODI ZA AL AHLY YA MISRI...ALICHOFANYA CHAWEKA HISTORIA...