Home Yanga SC ISHU YA DABI KUBADILISHWA TAREHE YANGA WATOA TAMKO

ISHU YA DABI KUBADILISHWA TAREHE YANGA WATOA TAMKO

 CEDRIC Kaze,Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa haoni tatizo ya mechi yao dhidi ya watani wa jadi Simba kubadilishwa tarehe na Bodi ya Ligi Tanzania.

Awali mechi hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na wadau wa masuala ya soka ndani na nje ya Bongo ilitarajiwa kuchezwa Februari 20.

Ila kwa sasa rasmi mechi hiyo imebadilishwa tarehe na itapigwa Mei 8,itakuwa ni ya mzunguko wa pili msimu wa 2020/21.

Ile ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Mkapa zama za Sven Vandenbroeck ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na vigogo hao waligawana pointi mojamoja.

Kaze amesema:”Sioni tatizo la mechi kupelekwa mbele kwani hilo limetokea na sitaweza kubadili kwa kuwa ni ratiba nina amini itafika na tutacheza ila kwa sasa acha tuweke nguvu kwenye mechi zetu zilizo mbele yetu,”

Februari 13, Yanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu ugenini mbele ya Mbeya City ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

Ule wa kwanza Uwanja wa Mkapa, Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44 ilishinda bao 1-0 lililopachikwa na Lamine Moro hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa Uwanja wa Sokoine. 

SOMA NA HII  YANGA V SIMBA FAINALI YA MAPINDUZI YAINGIZA MAMILIONI ZENJI