Home Uncategorized YANGA YATOA SABABU YA SARE NNE MFULULIZO ILIZOPATA NDANI YA LIGI KUU...

YANGA YATOA SABABU YA SARE NNE MFULULIZO ILIZOPATA NDANI YA LIGI KUU BARA


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya timu yake kuambulia sare kwenye mechi zake nyingi ni ujanja wa timu pinzani ndani ya Uwanja.

Yanga imeambulia sare nne mfululizo ilianza mbele ya Mbeya City kwa kufungana bao 1-1, Tanzania Prisons 0-0, Polisi Tanzania 1-1 na jana 0-0 mbele ya Coastal Union.

Eymael amesema kuwa :” Wachezaji wa timu pinzani wamekuwa ni mafundi wa kujiangusha na kupoteza muda bure jambo ambalo linapunguza kasi ya washambuliaji na wachezaji kupata matokeo,’.

Yanga imekusanya pointi 41 ipo nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 22.

SOMA NA HII  KIPA NAMBA MOJA SINGIDA UNITED AJIWEKA SOKONI