Home Uncategorized PAMOJA NA KUMCHAKAZA WILDER KWA TKO, FURRY ALIKUWA AMEONGOZA RAUNDI ZOTE SABA...

PAMOJA NA KUMCHAKAZA WILDER KWA TKO, FURRY ALIKUWA AMEONGOZA RAUNDI ZOTE SABA KWA POINTI




Tyson Fury amentwanga Deontay Wilder kwa TKO katika raundi ya saba baada ya kocha wa bondia huyo Mmarekani kulazimika kutupa taulo ulingoni.

Pamoja na kumchapa Wilder, Furry anayetokea nchini Uingereza imeonyeshwa aliongoza kwa raundi zote saba, hivyo alikuwa na nafasi ya kushinda kwa pointi pia.

Muda mwingi wa pambano hilo, Wilder aliyekuwa hajawahi kupoteza alikuwa akipokea makonde makali na raundi ya pili aliumia sikio watangazaji wakieleza alipasuliwa ngoma ya sikio.

Kwa sasa Furry maarufu kama The Gypsy amekamilisha kubeba mikanda yote mikubwa ya uzito wa juu akichukua huo wa WBC kutoka kwa Wilder. Kabla alikuwa na mikanda ya WBA, WBO, IBF na IBO ambao aliutwaa akimshinda Wladimir Klitschko.

SOMA NA HII  IBRAHIM AJIBU KWA SIMBA NDO BASI TENA MSIMU WA 2019/20