Home Uncategorized IBRAHIM AJIBU KWA SIMBA NDO BASI TENA MSIMU WA 2019/20

IBRAHIM AJIBU KWA SIMBA NDO BASI TENA MSIMU WA 2019/20


IBRAHIM Ajibu kiungo mshambuliaji ndani ya Simba kwa
msimu wa 2019/20 ndio basi tena ndani ya kikosi
hicho kuweza kuvunja rekodi yake aliyoweka msimu wa
2018/19 alipokuwa Yanga kwa kutoa jumla ya pasi 17 na
kufunga mabao sita.

Mambo yamekuwa magumu ndani ya Simba kwa kuwa
ameshindwa kuonyesha makeke yake kutokana na kutokuwa na namba kikosi cha kwanza kinachonolewa na
Sven Vandenbroeck.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 na kutwaa
ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2019/20 amecheza jumla
ya mechi 19 akitumia dakika 1,154 amefunga bao moja
na kutoa pasi tano za mabao kati ya 69.

Ana deni la mabao matano na pasi 12 ili aweze kuivunja
rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita ambapo haitawezekana tena kutokea kwa msimu huu wa 2019/20 kwa kuwa tayari umeshameguka mazima.

Mechi zake:-JKT Tanzania(13),Kagera Sugar (90),Biashara
United (77), Azam FC (6),Mwadui FC (30),Mbeya City
(80), Tanzania Prisons (55), KMC (63),Ndanda (90), Ruvu
Shooting (15),Mbao FC (85), Alliance (90), Namungo (56),
Coastal Union (63),Polisi Tanzania (45),JKT Tanzania (90)
Tanzania Prisons (45), Namungo,(71) na Mbao,(90).

SOMA NA HII  VIDEO:MASHABIKI WATAJA WACHEZAJI WALIOFANYA VIZURI LEO TAIFA, ISHU YA UBINGWA WAIGUSIA PIA