Home Uncategorized KENEDDY JUMA, JORDAN NA MOLINGA WAMALIZA LIGI NA REKODI ZAO

KENEDDY JUMA, JORDAN NA MOLINGA WAMALIZA LIGI NA REKODI ZAO


JULAI 26, majalada ya Ligi Kuu Tanzania Bara yalifungwa rasmi kwa michezo 10 kuchezwa huku kila timu ikivuna kile ilichopanda ndani ya dakika 90.
Ukiachana na Alliance FC, Lipuli,Ndanda na Singida United kushuka daraja huku Mbao FC na Mbeya City zikipata nafasi ya kucheza playoffs leo, Kenned Juma wa Simba na Jordan John wa Mbao FC walimaliza msimu na rekodi zao za kibabe.
Kwenye mchezo wa Simba mbele ya Polisi Tanzania, Juma alitengeneza pasi ya bao kwa John Bocco la kuongoza kwa Simba dakika ya pili kisha akawazadia Polisi Tanzania penalti dakika ya 45 baada ya kumchezea rafu Anthon Matheo ndani ya box na Marcel Kaheza alimtungua Manula.
Wakati Juma akihusika kwenye mabao yote mawili ya Simba na Polisi Tanzania, Jordan wa Mbao inayonolewa na Felix Miziro alifunga bao la kali la nje ya 18 lililowahakikishia kucheza playoffs leo kwa kumtungua Ally Mustapha wa Ndanda ambao wameshashuka daraja.
David Molinga wa Yanga naye alifunga bao lake la 11 kwa kuifunga Lipuli lililoishusha jumla timu hiyo Uwanja wa Samora lililowapa pointi tatu Yanga ambao wapo nafasi ya pili na pointi 72.
SOMA NA HII  MITAMBO MITATU YA MABAO SIMBA KUIKOSA POLISI TANZANIA LEO