Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU…MATOLA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA HALI ILIVYO...

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA RUVU…MATOLA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA HALI ILIVYO NDANI…


Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja kwa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Matola amesema baada ya kurudi kutoka mkoani Lindi katika mchezo dhidi ya Namungo kikosi kiliingia kambini moja kwa moja tayari kwa mtanange huo.

Matola amesema hatujapata ushindi katika michezo mitatu iliyopata lakini jambo hilo halijashusha morali yetu na tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Ruvu ni timu nzuri na ipo kwenye nafasi mbaya katika msimamo hivyo wanahitaji ushindi ili kujinasua lakini tupo tayari kuwakabili.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri wachezaji wote wapo tayari isipokuwa Hassan Dilunga na Sadio Kanoute ambao ni majeruhi,” amesema Matola.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI