Home news SIMBA YA MO DEWJI WAAMUA KUFANYA KWELI AFRIKA…WACHEZAJI WATENGEWA BILIONI 1.4 KAMA...

SIMBA YA MO DEWJI WAAMUA KUFANYA KWELI AFRIKA…WACHEZAJI WATENGEWA BILIONI 1.4 KAMA BONASI TU..INAANZA LEO..


SIMBA SC, imepania kweli kufika mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mabosi wa klabu hiyo, wametenga dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 230 za Kitanzania) kila timu ikiibuka na ushindi kuanzia sasa Timu hiyo ambayo leo Jumapili itaanza mechi za hatua ya makundi kwa kucheza dhidi ya ASEC Mimosas kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, itakuwa na mechi sita za hatua hiyo kabla ya kwenda robo fainali.

Katika mechi hizo sita za hatua ya makundi zikiwa tatu nyumbani na nyingine ugenini, mabosi hao wa Simba wamesema kila mechi ushindi ukipatikana, wachezaji watapewa kiasi hicho cha fedha ambapo wakishinda zote sita, jumla zitakuwa dola 600,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.4 za Kitanzania.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimesemakwamba: “Usituone sisi huwa tunanenepa sana tunapoanza michuano ya kimataifa, hii yote ni kwa sababu bonasi nzuri ambazo viongozi wetu huwa wanatuwekea mezani.

“Kwa mfano hivi sasa tunapokwenda kucheza mechi za hatua ya makundi, tumewekewa dola 100,000 kila tukishinda mechi jambo ambalo tuna uhakika nalo tutazipata kutokana na malengo yaliyopo.

“Cha kufurahisha zaidi hadi sasa viongozi wameshatenga pembeni pesa hizo na tunachotakiwa ni sisi kupata ushindi na mara moja tunapewa fedha zetu, hakuna kusubiri, yaani baada ya mechi, mzigo unatoka.”

Alipotafutwa  Mratibu wa Simba, Abas Ally ili afafanue juu ya hilo, ambapo alisema: “Ni kweli sisi kila mwaka tunapoingia katika michuano ya kimataifa huwa tunapata bonasi ya dola laki moja, safari hii tumeshahakikishiwa kuzipata mapema iwezekanavyo na ndiyo maana mimi huwa najisikia vibaya sana ninapoona watu wakimdharau bosi wetu Mohamed Dewji kwani anaisaidia sana timu yetu.”

Ikumbukwe kuwa, malengo ya Simba msimu huu katika michuano hiyo ni kufika nusu fainali, huku wakipanga kuhakikisha wanashinda mechi zote tatu za nyumbani katika hatua ya makundi ambapo wakifanikiwa katika hilo, watakuwa na uhakika wa kupata bonasi ya dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 691 za Kitanzania). Soma ukurasa wa 15 kufahamu kwa kina mchezo huu kati ya Simba dhidi ya ASEC Mimosas.

SOMA NA HII  LUIS MIQUISSONE AFUNGUKA MASHABIKI KUMFANANISHA NA MESSI