Home Uncategorized MTIBWA SUGAR:MECHI YETU MBELE YA MBEYA CITY ILIKUWA NYEPESI KWELI

MTIBWA SUGAR:MECHI YETU MBELE YA MBEYA CITY ILIKUWA NYEPESI KWELI


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa mechi yake mbele ya Mbeya City ilikuwa nyepesi kwao licha ya kichapo cha bao 1-0 walichokipata.

Februari 22, Mtibwa Sugar ilimenyana na Mbeya City Uwanja wa Sokoine na ilipoteza kwa bao la penati lililofungwa na Peter Mapunda.

Katwila amesema:”Mchezo wetu dhidi ya Mbeya City kwetu ulikuwa mwepesi na wachezaji walifanya kazi kubwa uwanjani, tumefungwa bao moja tu na lenyewe ni la penalti.

“Siwezi kuwalaumu sana wachezaji kwani juhudi uwanjani walionyesha na wanastahili pongezi tunachokifanya kwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,” amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 ina pointi 24 ikiwa imecheza mechi 24.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO