Home Uncategorized YANGA YATUA KWA BEKI MRWANDA

YANGA YATUA KWA BEKI MRWANDA


 BAADA ya Yanga kumkosa beki wa kushoto, Eric Rutanga katika dakika za mwisho za usajili uliopita, hatimaye uongozi wa Yanga umerudi tena kwa Mnyarwanda huyo kwa ajili ya kumsajili kuja kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi wa kushoto la timu hiyo.

 

Yanga katika eneo la ulinzi wa kushoto kwa sasa kuna wachezaji wawili ambao ni Yassin Mustapha na Adeyum Saleh huku Yassin Mustapha akionekana kupata nafasi ya kucheza mara nyingi kumzidi Adeyum.

 

Rutanga, raia wa Rwanda, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Polisi ya nchini humo ambapo hapo awali alikuwa akikipiga katika Klabu ya Rayon Sports kabla ya kuhamia Polisi United.

 

Beki huyo amesema kuwa viongozi wa Yanga wameanza kumtafuta tena hivi karibuni wakiangalia uwezekano wa yeye kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la usajili.

 

“Nikiwa Rayon Sports nilitakiwa nijunge na Yanga ambao tayari tulikuwa tumeshakubaliana kwa mambo mengi lakini mwisho wa siku mambo hayakunyooka.


 “Katika dirisha hili dogo la usajili naona Yanga wamerudi tena, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hili jambo, tutaona litakavyokuwa,” amesema beki huyo.


Yanga kwenye safu ya ulinzi imeweza kuwa imara kwenye mechi zake 14 ambapo imeruhusu kufungwa mabao matano ndani ya dakika 1,260.


Ina wastani wa kuruhusu bao moja kila baada ya dakika 252 kwa msimu wa 2020/21 ipo nafasi ya kwanza na pointi zake 34.

SOMA NA HII  Kandanda.co.tz ipo pamoja na Taifa Stars