Home news BAADA YA KUONA KIWANGO CHA SAKHO SIKU ZA HIVI KARIBUNI…PABLO AKUNA KICHWA...

BAADA YA KUONA KIWANGO CHA SAKHO SIKU ZA HIVI KARIBUNI…PABLO AKUNA KICHWA WEE…KISHA ANENA HAYA..

 


KOCHA wa Simba, Pablo Franco ameyaelewa sana mavitu ya fundi, Ousmane Sakho.

Pablo huwezi kumwambia kitu juu yake kwa namna anavyopambana ndani ya uwanja kuipa timu yake matokeo na amesisitiza si yeye tu kijumla morali ya wachezaji wa Simba iko juu.

Sakho ni miongoni mwa mastaa waliowashika mashabiki wa Msimbazi kwa sasa kutokana na kipaji chake na umuhimu wake kwenye kikosi cha kwanza cha Mnyama.

Kiufundi amekuwa na mchango mkubwa ndani ya timu hiyo kwa sasa tofauti na wenzake Sadio Kanoute pamoja na Peter Banda ambao wote walisajiliwa wakati mmoja huku Duncan Nyon ambaye akifungashiwa vilago katika dirisha dogo lililofungwa jana usiku.

Akizungumza na  Gazeti la Mwanaspoti Kocha Pablo alisema, Sakho ni mchezaji ambaye kila uchao kiwango chake kinakuwa bora zaidi hivyo hata yeye anafurahi kuwa na mchezaji wa aina hiyo na anajivunia.

lisema Sakho alipotua Simba na sasa amekuwa tofauti na kila mchezo anakuwa na vitu vipya ambavyo mbali na mashabiki kufurahi pia vina mchango mkubwa ndani ya timu.

“Sio Sakho peke yake, Simba ina wachezaji wengi na wote wana uwezo mkubwa, lakini kwa kuwa umeniuliza Sakho ni mchezaji mzuri na anajituma dakika zote atakazocheza na juhudi zake zina faida kwa timu,” alisema Pablo.

Pablo alisema anapenda kuona wachezaji kila mmoja akibadilika alipo na kwenda hatua nyingine kwa kuwa inampa nafasi yeye ya kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi pale kunapokuwa na mechi.

WANACHAMA WATOA NENO

Wanachama wa Simba kindakindaki Daudi Simba kutoka Kamati ya Roho Mbaya alisema, Sakho alianza kuziba pengo la Chama na wao walikuwa wamekubali yaishe na kuanza kumsahau.

“Angalia hapa Sakho kule Chama au Morrison aisee watu wataita maji mma, timu sio ya mchezo, sema kwenye safu ya ulinzi tunahitaji kuboresha pia,” alisema.

Justine Joel kutoka Wekundu wa Terminal alisema, hana wasiwasi na mchezaji yoyote ndani ya klabu yao, kutokana na kila mmoja kuwa na uwezo ambao anaimani wataisaidia timu.

SOMA NA HII  WAKATI BODI YA LIGI WAKIIKATALIA SIMBA KUCHEZA NA COSTAL...MBRAZILI KAAMUA KUJA NA GIA HII...

“Watani wajipange kusema ukweli, hii Simba Next levo huyu Sakho ana raha yake lakini Mwamba wa Lusaka hana mpinzani buana,” alisema Justine.