Home Uncategorized NYOTA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED APATA CORONA

NYOTA WA ZAMANI WA MANCHESTER UNITED APATA CORONA


MAROUANE Fellaini, kiungo wa zamani wa Klabu ya Manchester United anayekipiga ndani ya Klabu ya Shandong Luneng ya China amegundulika na Virusi vya Corona.

Nyota huyo mwenye miaka 32 anakuwa mchezaji wa kwanza kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu ya China kugundulika na Virusi vya Corona aligundulika Ijumaa katika Hospitali iliyopo mjini Jinan na mpaka anagundulika na Virusi hivyo hakuonyesha dalili zozote kwamba hayupo salama.

Kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktri maalumu ambao wanampa huduma nyota huyo ili arejee kwenye ubora wake katika eneo maalumu lililopo ndani Jinan Hospitali.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na timu yake ya Shandong Luneng raia huyo wa Ubelgiji hakuwa na dalili zozote za Corona.

Fellain amesema anawashukuru mashabiki kwa kuwa naye bega Kwa bega anaamini atarejea kwenye shughuli zake kama kawaida kutokana na huduma alizopata.

SOMA NA HII  TAZAMA HAPA LIIVE MECHI YA CONGO DHIDI YA UGANDA - AFCON 2019