Home Uncategorized TAMKO LA TTF KUHUSU MOLINGA NA EYMAEL LAIVURUGA YANGA

TAMKO LA TTF KUHUSU MOLINGA NA EYMAEL LAIVURUGA YANGA

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa iwapo tamko la Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) litaamua kuwazuia wachezaji waliovuka mipaka ya Tanzania kutokucheza mechi za Ligi Kuu Bara kutawavurugia mipango yao kutokana na baadhi ya wachezaji wake kuondoka.

Wallace Karia ambaye ni Rais wa TFF alisema kuwa hakuna mchezaji atakayepewa ruhusa ya kucheza iwapo alitoka nje ya nchi kwa kuvuka mipaka kwa muda huu ambao Ligi Kuu Bara imesimamishwa.

“Hakuna ambaye amepewa ruhusa ya kuondoka nje ya ya nchi kwani sio likizo bali ni sitisho kwa muda kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya Virusi ya Corona hivyo kwa mchezaji ambaye atatoka nje ya nchi hataruhusiwa kucheza mechi zote ambazo zitaendelea ili kujikinga zaidi,” alisema Karia.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa iwapo tamko hilo litakuwa hivyo watapata athari kutokana na mchezaji wao Molinga (David) na Kocha Mkuu, Luc Eymael kuwa nje ya nchi.

“Tutaathirika kutokana na tamko hilo kwani Molinga na Kocha Mkuu hawapo nchini kwa sasa tuliwapa ruhusa hivyo tutakachokifanya ni kuwasiliana na TFF ili kujua namna gani tutaliweka sawa jambo hili ikishindikana basi hatutakuwa na na namna nyingine,” amesema.

SOMA NA HII  KUMBE UJANJA WANAOTAMBA NAO YANGA UKO HAPA