Home Uncategorized WACHEZAJI NAMUNGO WAIBUKIA BONGO

WACHEZAJI NAMUNGO WAIBUKIA BONGO

WACHEZAJI na Viongozi wa timu ya Namungo FC ya Ruangwa inayotumia Uwanja wa Majaliwa wametimka Ruangwa na kuibukia Bongo ili kumalizia mapumziko ya muda yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kujizuia na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Machi 17, Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilizuia mijumuiko yote isiyo ya lazima ili kujikinga na maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona ambapo Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake zimesimamishwa kwa muda wa siku 30.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Namungo FC,Hitimana Thiery amesema kuwa wachezaji wote wameondoka Ruangwa na kuibukia Bongo ili kuendelea kuchukua tahadhari ya Corona.
“Hatupo kwa sasa Ruangwa, niliondoka na wachezaji kutoka Ruangwa lengo ikiwa ni kutumia muda huu wa kupambana na maambukizi ya Corona kwa kila mmoja kuwa sehemu ambayo ni salama zaidi kwake na wengi wamechagua kutulia Bongo na tahadhari wamepewa kwani virusi hivi sio kitu cha kuchukulia utani,” amesema Thiery. 
SOMA NA HII  MASHABIKI TUNAPASWA TUWE WASIKIVU, TUACHE UKOROFI NA KIBURI KATIKA KUFUATA MUONGOZO