Home Habari za michezo WAKATI WAKIJIANDANA MECHI IJAYO…’GONJWA’ JIPYA LAGUNDULIKA SIMBA…MATOLA AVUNJA UKIMYA…

WAKATI WAKIJIANDANA MECHI IJAYO…’GONJWA’ JIPYA LAGUNDULIKA SIMBA…MATOLA AVUNJA UKIMYA…


IKIWA imecheza michezo mitano kimataifa katika hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, rekodi za Simba upande wa kona zinasikitisha kwa kuwa zimekuwa hazina faida kwao.

Ndani ya dakika 450, walipata kona 24 na katika kubadili mapigo hayo huru kuwa mabao, ilikuwa ni ngumu kwa wawakilishihao wanaofundishwa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kwa kuwa walifunga bao moja lililosababishwa na kona.

Ni kona moja iliweza kuleta bao ilipigwa na Shomari Kapombe mbele ya USGN ya Niger huku mtupiaji akiwa ni Bernard Morrison raia wa Ghana.

Wapigaji wa kona kwa Simba ni Rally Bwalya ambaye kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas uliochezwa Uwanja wa Mkapa alipiga jumla ya kona 6.

Mwingine mwenye kazi ya kupiga kona ni Kapombe ambaye kwenye mashindano ya kimataifa ana pasi mbili na alifunga bao moja kwa mkwaju wa penalti.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba alisema kuwa, makosa ambayo yanatokea uwanjani wanayafanyia kazi uwanja wa mazoezi.

“Makosa yapo hasa kwenye mechi zetu ambazo zimepita tumeona ikiwa ni pamoja na matumizi ya mapigo ya kona hivyo kwenye sehemu ya mazoezi tutafanyia kazi,” alisema.

SOMA NA HII  CAF WAIPIGA 'JEKI KIMTINDO' TAIFA STARS KUFUZU MASHINDANO YA CHAN....WASHINDWE WAO TU SASA...