Home Uncategorized SERBIA MAMBO BADO MAGUMU, CORONA YASIMAMISHA KILA KITU

SERBIA MAMBO BADO MAGUMU, CORONA YASIMAMISHA KILA KITU


NASORRO Mohamed nyota wa Tanzania anayekipiga kwenye Klabu ya OFK Zarkovo ya nchini Serbia inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza amesema kuwa kutokana na hofu ya kusambaa kwa virusi vya Corona shughuli zote nchini Serbia zimesimamishwa.
Nyota huyo ambaye alipata dili hilo akitokea klabu ya vijana ya Mtibwa Sugar alikwea pipa Februari 29 pamoja na Abdalah Shaibu ‘Ninja’ ambaye yeye anakipiga OFK Vyskor kwa mkopo baada ya kupewa dili la miaka miwili na Klabu ya MFK Vyskor.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mohamed alisema kuwa kwa sasa hakuna kinachofanyika ndani ya nchi ya Serbia kutokana na hofu ya virusi vya Corona.
“Huku tunamshukuru Mungu tupo salama ila hakuna kinachofanyika kwa sasa kwani hofu sio kubwa lakini shughuli zote zimesimama hivyo hakuna kinachoendela wakati huu,” alisema Mohamed.
SOMA NA HII  DUKE ABUYA AIPIGA MKWARA YANGA