Home Uncategorized KILICHO NYUMA YA SARESARE ZA TANZANIA PRISONS HIKI HAPA

KILICHO NYUMA YA SARESARE ZA TANZANIA PRISONS HIKI HAPA

KOCHA wa timu ya Tanzania Prisons, Adolf Rishard amesema mfumo wake kueleweka kwa wachezaji wake ni jambo lililokuwa linampa matokeo akiwa uwanjani.

Prisons inaongoza kwa timu ngumu kutoa matokeo ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya tisa na pointi 40 kutokana na kutoa sare nyingi ikiwa nazo 13 huku Simba ikiwa ni ya mwisho kwenye timu zenye sare ikiwa nazo mbili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Rishard amesema kuwa amekuwa akiongea na wachezaji wake mara kwa mara ili kuwajenga kisaikolojia pale wanapopata nafasi ya kuanza kucheza mechi zao.
“Wachezaji wanatambua kazi yao wakiwa uwanjani ni kutafuta ushindi inategemea na aina ya timu ambayo ninakutana nayo uwanjani na kazi yao inakuwa moja kupambana kutafuta matokeo ndio maana tumekuwa tukiambulia pointi,” amesema.
Timu zinazoshika nafasi tatu za juu ikiwa ni Yanga, Azam FC  na Simba zote zimekutana na moto wa Prisons ambapo ziliambulia sare kwenye mechi walizokutana na Rishard.
SOMA NA HII  SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI POLISI TANZANIA