Home Uncategorized SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI POLISI TANZANIA

SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI POLISI TANZANIA


BAADA ya Simba kutia timu Moshi, leo kikosi cha Simba kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 26 Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Taifa,  Simba ilishinda mabao 2-1 na kusepa na pointi tatu mazima. 

Hakuna timu yenye presha ya kushuka ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 zote zina uhakika wa kubaki ndani ya ligi.

Simba inayoongozwa na Sven Vandenbroeck ipo  nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 84 na imeshakabidhiwa ubingwa.

Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 55 kibindoni zote zimecheza mechi 37.

SOMA NA HII  KMC YATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA