Home Uncategorized ISHU YA PAPY TSHISHIMBI KUIBUKIA SIMBA IMECHORWA HIVI,SABABU ZATAJWA

ISHU YA PAPY TSHISHIMBI KUIBUKIA SIMBA IMECHORWA HIVI,SABABU ZATAJWA


PAPY Tshishimbi, nahodha wa zamani wa Yanga amesema kuwa hana tatizo ikiwa Simba watamfuata ili asaini dili jipya ndani ya klabu hiyo.

Tshishimbi kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na mabosi zake wa zamani, Yanga baada ya mkataba wake kuisha na hakuongezewa mkataba mwingine.

Habari zinaeleza kuwa Simba inahitaji kuinasa saini ya Tshishimbi kutokana na madai ya usumbufu na utovu wa nidhamu wa mara kwa mara kutoka kwa kiungo mkongwe wa timu hiyo, Jonas Mkude, hivyo Papy analetwa kwa lengo la kumpa changamoto.

 

Kingine ni kwamba wameona hakuna haja ya kumleta mchezaji mwingine kutoka nje na Tanzania, ambaye atakuja kuanza upya, hivyo Papy amepewa nafasi kubwa kwa kuwa ni mchezaji huru, lakini pia ameshaijua ligi ya Bongo na anayafahamu vema mazingira ya soka.

 

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba, uongozi wa timu hiyo utakamilisha mazungumzo ya kumsajili kiungo huyo wakati wowote huku wakiwa wamepanga kumpa mkataba wa miaka miwili.

 

“Suala la mazungumzo na Tshishimbi yapo na yanakwenda vizuri kwa sababu uongozi umedhamiria kumleta Simba na ukiangalia yule ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.

 

“Mkakati uliopo ni kumpa mkataba wa miaka miwili na tayari mkataba upo, tayari umeshaandaliwa, ndiyo maana nakwambia haziwezi zikapita siku mbili atakuwa ameshatambulishwa na kuna mambo mengi ya kiufundi yameangaliwa ili timu iweze kupata faida na siyo jambo ambalo watu wamelikurupukia,” kilisema chanzo hicho.


 Tshishimbi amesema:”Naweza kwenda popote pale ambapo nitatakiwa kwenda kucheza kwani mimi ni mchezaji na nipo huru ukizungumzia soka ndiyo kazi yangu sina tatizo katika kucheza.


“Mpaka sasa nina ofa nyingi mkononi hivyo ikikamilika itajulikana wapi nitakuwa kwa ajili ya msimu ujao.”



SOMA NA HII  CHAMA NAE AONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA MSIMBAZI..... ISHU IKO HIVI