Home Burudani MWAKINYO AFANYA HAYA KWENYE ADHABU YA MANARA TFF

MWAKINYO AFANYA HAYA KWENYE ADHABU YA MANARA TFF

Mwakinyo na Manara

Bondia wa ngumi za kulipwa Tanzania, @hassanmwakinyojr amemuombea msamaha Haji Manara kwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kumsamehe adhabu yake.

Manara amefungiwa miaka miwili kujihusisha na masuala ya soka na mpaka sasa ametumikia mwaka mmoja na amebakisha mwaka mmoja katika kifungo chake.

Mwakinyo alianza kuandika; “Asema ajabal liamri muumin, Inna amruhu quluh lahu, khairun walaysa zalka lia ahadin, ila lil muumin inn aswabatuh saraa shakar, faqana khaira llah inn aswabatuh Daraa swabaru faqana khaira llah

“Ajabu ya amri ya muumin hakika jambo lake lote kwake yeye ni kheri, akipatwa na jambo la kufurahisha kwake yeye ashukuru Mungu ni kheri kwake akipatwa na jambo la mauzi na la kuchukiza ashukuru Mungu pia ni kheri, kwake.

“Wakati mwingine Mungu hufanya mambo kuwa kinyume chake hukunyima ili akupe na hukupa ili akunyime. Binafsi Nimepatwa na huzun sana na huruma ya kibinaadam juu ya anayo yapitia bwana huyu nimeskilza baadhi ya mahojiano yake ameongea kwa hisia sana na uchungu wa mwisho kabisa!

“Kua binaadam ambae una mapungufu na huyaoni mapungufu yako tayari nikupungukiwa lakini haikutoi kwenye ubinaadam siko hapa kuchochea chochote lakin maneno ya haji yameniuma sana kama binaadam.

“Ni ukweli ana mchango wake mkubwa sana kwenye soccer letu, binafsi mimi na wengine wengi tulikua tunajua mpira ni kwa ajili ya wazee tu na sio vijana mimi nimejua mpira kupitia haji na mchango wa haji mkubwa umefanya tujue mpira ni haki ya kila mtu.

“Everyone makes mistakes, that’s life naomba sana walezi wa soccer la taifa letu TFF wamfikirie bwana haji ambae nusu ya maisha yake ametumikia soccer na ndio ulipo ugali wa yeye na family yake yupo Mama, wapo watoto ipo family kamili inayo mtizamia kama BaBa.

“Natumai TFF ina viongozi wasikivu na waungwana sana wa kiongozwa na rais wallace karia nakiri kua adhabu walio kupa ni katika kukujenga tu haina maana watu wanakuchukia au kutaka wafike ulipo…. @taifastas_tff #vivabugati,“ aliandika Mwakinyo.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AJA NAKULI HII SIMBA