Home Uncategorized BEKI SIMBA AKUBALI UWEZO WA SAIDO WA YANGA

BEKI SIMBA AKUBALI UWEZO WA SAIDO WA YANGA

 


BONIFACE Pawasa, beki wa zamani wa Simba, amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibazonkiza ni habari nyingine kwenye soka la Bongo kutokana na uwezo alionao.

 

Ntibazonkiza ni ingizo jipya ndani ya Yanga akiwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, amefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao.

 

Mchezo wake wa kwanza ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji ambapo alifunga na kutoa pasi moja na mchezo wa pili ulikuwa ni dhidi ya Ihefu, hapo alitoa pasi mbili za mabao.

 

Pawasa amesema kuwa amemtazama nyota huyo kwenye mechi alizocheza na kugundua kwamba ni miongoni mwa usajili mzuri uliofanywa na Yanga kwa miaka ya hivi karibuni.

 

“Ntibazonkiza ni mchezaji mzuri, kwa aina yake ya uchezaji anaonekana kuwa imara kwa sababu hana uchoyo wa pasi na anajua kutengeneza nafasi, hivyo mabeki lazima wawe makini wanapokutana naye kwani muda wowote anaweza kubadili matokeo.

 

“Kuwa na mchezaji ambaye ana uwezo wa kubadili matokeo muda wowote ni hazina kwa timu. Ninaamini kwamba ikiwa hatapata majeraha kwa wakati huu kutakuwa na mengi ambayo atayafanya ndani ya uwanja,” amesema Pawasa.


Chanzo:Spoti Xtra

SOMA NA HII  BALINYA AMTIKISA KAGERE BONGO