Home Uncategorized HUYU HAPA AMESHIKILIA PANGA LA KUWAPIGA CHINI WACHEZAJI SIMBA NA KULETA MASHINE...

HUYU HAPA AMESHIKILIA PANGA LA KUWAPIGA CHINI WACHEZAJI SIMBA NA KULETA MASHINE MPYA

Habari za Michezo leo


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa uliopo kwa timu ni kufanya vema kwenye mashindano watakayoshiriki huku suala la usajili pamoja na kuwaacha wachezaji likiwa mikononi mwa Kocha Mkuu, Sven Vandernbroeck.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mbatha amesema kuwa hesabu kubwa ni kuona wanafikia malengo ambayo wamejiwekea ambayo ni kutwaa ubingwa huku suala la usajili likiwa kwa kocha.

“Tuna mpango wa kufanya vizuri kwenye mechi zetu ambazo tutacheza kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho pamoja na lile la Ligi Kuu Bara sasa ili hayo yafanikiwe ni lazima kuwe na maandalizi.

“Kwa upande wa usajili mipango ipo na itategemea ripoti ya kocha ambaye yeye anajua aina ya wachezaji anao wahitaji hivyo katika hili mashabiki wawe na subira,” amesema.

SOMA NA HII  BARAKA MAJOGORO AZIINGIZA VITANI YANGA NA SIMBA