Home Habari za michezo YANGA KUTUMA UJUMBE AFRIKA NZIMA JUMAPILI HII, ALLY KAMWE ATAMBA

YANGA KUTUMA UJUMBE AFRIKA NZIMA JUMAPILI HII, ALLY KAMWE ATAMBA

Ofisa Habari wa Klabu ya Young Africans Sports, Alikamwe amesema kuwa watakachokwenda kukifanya dhidi ya wapinzani wao ASAS FC siku ya Jumapili zitakuwa ni salamu tosha kwa Afrika na kuitambua timu hiyo.

“Tunachokwenda kukifanya Jumapili dhidi ya ASAS FC inatakiwa Afrika ijue kuwa sisi Yanga SC ndio mabingwa wa Tanzania,” amesema Ally Kamwe.

Kamwe amewataka mashabiki wa soka, wapenzi na wanachama kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwenda kutoa sapoti yao kwa Wananchi watakapokuwa wakiipeperusha bendera ya Taifa pale Azam Complex Chamazi

”Mashabiki twendeni tukaujaze uwanja lakini pia kikosi chetu kinakwenda kuwakumbusha watu kuwa sisi ndio mabingwa watetezi na hivi ndivyo tunavyotoa salamu zetu,” amesema Kamwe.

Young Africans Sports watatupa karata yao ya kwanza kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika dhidi ya ASAS ya Djibout siku ya Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex Chmazi.

SOMA NA HII  SIMBA WAFANYA KWELI ...UZI MPYA WA KIMATAIFA N BALAH NA NUSU...