Home Uncategorized ARSENAL YAMPIGA MKWARA WA KIMTINDO AUBAMEYANG

ARSENAL YAMPIGA MKWARA WA KIMTINDO AUBAMEYANG

MIKEL Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa hawezi kumbembeleza mchezaji kusalia ndani ya klabu hiyo iwapo hana nia ya kubaki hapo.

Hali hiyo imefikia kutokana na kuwepo tetesi kwamba nyota wao Pierre Emerick Aubameyang amegoma kusaini dili jipya.

Mkataba wake ndani ya Arsenal umebakiwa na miezi 14 kabla ya kumeguka kikosini hapo na unatarajiwa kumalizika mwezi Juni 2021.

Imekuwa ikitajwa kuwa Inter Milan, Barcelona na Real Madrid zinahitaji kupata saini ya mshambuliaji huyo ambaye ni nahodha ndani ya Arsenal. “Siwezi kumshawishi mchezaji kucheza Arsenal au kujiunga na sisi, mchezaji anatakiwa kujituma na kujitoa kwa ajili ya klabu,” amesema.

SOMA NA HII  KLOPP SASA ANAFIKIRIA KUMVUTA KOULIBALY