Home Uncategorized KOCHA NDANDA AHOFIA VIJANA WAKE KUTOKA KWENYE RELI

KOCHA NDANDA AHOFIA VIJANA WAKE KUTOKA KWENYE RELI



ABDUL Mingange, Kocha Mkuu wa Ndanda FC amesema kuwa kusimamishwa kwa Ligi Kuu Bara kwa muda wa mwezi mmoja kutawatoa wachezaji wake kwenye reli kutokana na kasi waliyoanza kuitengeneza.

Ndanda FC ilikuwa imerejea kwenye ubora wake ambapo kwa mwezi Februari, Mingange aliingia kwenye kuwania tuzo ya Kocha Bora wa mwezi huku mchezaji wake Vitalis Mayanga akiibuka mchezaji bora wa mwezi.
Kwenye mechi zake saba alizoongoza  mwezi Februari alifungwa moja na alishinda tano na kulazimisha sare  mbili matokeo yake yalikuwa namna hii:- Februari 1, Ndanda 1-0 Alliance, Februari 5, Ndanda 3-0 Mbao, Februari 8, Ndanda 0-0 Namungo, Februari 11, Mwadui 0-2 Ndanda, Februari 15 Singida United 0-1 Ndanda, Februari 19, Ndanda 1-1 Azam FC, Februari 22, Ndanda 2-1 KMC, Februari 29, Mtibwa Sugar 2-0 Ndanda.
Mwezi Machi Ndanda ilicheza mechi nne na ililazimisha sare mechi mbili na ilishinda moja na kupoteza mchezo mmoja pia, matokeo yake:-Machi 4, Lipuli 3-3 Ndanda, Coastal Union 0-0 Ndanda, Ndanda 2-1 Kagera Sugar na Polisi Tanzania 1-0 Ndanda kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa ilipaswa icheze na Biashara United.
Mingange amesema kuwa kusimamshwa kwa ligi kwa sababu ya kupambana na Virusi vya Corona ni jambo la msingi kutokana na umuhimu wa afya lakini ana mashaka na vijana wake kuweza kurejea kwenye kasi ambayo walikuwa nayo.
SOMA NA HII  SIMBA YAMPELEKA MCHEZAJI YANGA HOSPITALI