Home Uncategorized MOHAMED SALAH AFUNGUA AKAUNTI MPYA HUKO ENGLAND

MOHAMED SALAH AFUNGUA AKAUNTI MPYA HUKO ENGLAND


MOHAMED Salah, mshambuliaji wa Liverpool ameanza kwa kasi msimu mpya wa Ligi Kuu England 2019/20.

Salah raia wa Misri anayekipiga pia kwenye timu ya Taifa amefungua akaunti mpya ya kupachika mabao ndani ya Ligi Kuu England.

Mechi ya kwanza iliyochezwa Jana Ijumaa Uwanja wa Anflied, Liverpool iliwanyoosha mabao 4-1 wapinzani wao Norwich City.

Salah alifungua akaunti yake dakika ya 19 akimalizia pasi ya Robert Firmino.

Huu ni mwanzo mzuri kwa nyota huyo ambaye msimu uliopita aliibuka mfungaji bora ndani ya Ligi Kuu England baada ya kupachika jumla ya mabao 22.

SOMA NA HII  ARSENAL YAMPIGIA HESABU BEKI WA DORTMUND