Home kimataifa LUKAKU AKWEA PIPA KUIBUKIA LONDON

LUKAKU AKWEA PIPA KUIBUKIA LONDON


 MSHAMBULIAJI wa Inter Milan Romelu Lukaku anakwea pipa kuelekea London kwa ajili ya kukamilisha dili la kujiunga na Chelsea.

Dau ambalo amewekewa mezani ni Euro milioni 115 ili kukamilisha uhamisho wake kutoka Inter Milan kuelekea Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu England.

 Nyota huyo mwenye miaka 28 atakamilisha masuala ya vipimo kabla ya kusaini dili jipya kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo.

Anatarajiwa kusaini dili la miaka mitano kwa ajili ya kuitumikia timu yake hiyo ya zamani ambayo alicheza hapo kabla ya kusepa mwaka 2014.


SOMA NA HII  VIDEO: SIMBA YAITANGAZIA KIAMA YANGA, NABI AFUMUA KIKOSI KISA CHAMA