Home Uncategorized YANGA YATOA RAMANI NZIMA YA KUSEPA NA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

YANGA YATOA RAMANI NZIMA YA KUSEPA NA UBINGWA WA LIGI KUU BARA


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kuendelea kushinda mechi zote ambazo zimebaki ndani ya Ligi Kuu Bara.


Yanga imeshinda jumla ya mechi 11 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa na sare nne kwenye mechi 15 ambazo imecheza.


Leo itakuwa na kazi Uwanja wa Liti, kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United kwa ajili ya kujiweka sawa majira ya saa 10:00 jioni.


Kaze ametoka kushinda mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui kwa ushindi wa mabao 5-0 jambo lililowafanya wazidi kujikita kileleni na pointi zake 37.


Kocha huyo kipenzi cha mashabiki amesema:”Bado kuna kazi kubwa ya kufanya mpaka kufikia ubingwa ulipo na inawezekana kufanya vizuri kwa sababu tuna mwendo makini.


“Kwenye kila mchezo kwetu ni fainali na tutapambana ili kupata matokeo mazuri, mashabiki watupe sapoti ili tuweze kufikia malengo yetu,” .


Yanga imefunga jumla ya mabao 22 na kinara wa utupiaji wa mabao ni Michael Sarpong mwenye mabao manne.

SOMA NA HII  KOCHA AMPELEKA HAALAD APELEKWA REAL MADRID