Home Yanga SC MUANGOLA WA YANGA AMPOTEZA LUIS NDANI YA BONGO

MUANGOLA WA YANGA AMPOTEZA LUIS NDANI YA BONGO

 

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola mabao yake matatu yamempoteza mshikaji wake Luis Miquissone wa Simba mwenye mabao mawili katika kucheka na nyavu ndani ya uwanja licha ya kutumia dakika kiduchu.


Luis amecheza jumla ya mechi 14, mechi 9 ameyeyusha dakika 90 zote na kumfanya atumie dakika 810 huku mechi tano akitumia jumla ya dakika 383. Jumla ametumia dakika 1,193 akikosekana kwenye mechi nne.

 Mabao yake mawili kati ya 42 ambayo yamefungwa na Simba, aliwafunga JKT Tanzania na kushangilia kwake kulisababishwa aonyeshwe kadi ya njano.Bao la pili aliwafunga Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

Wakati Luis akifanya yake, Carlinhos amefunga matatu kwenye mechi sita ambazo amecheza kati ya mabao 34 yaliyofungwa na timu yake. Ametumia jumla dakika 346 na ni mechi mbili pekee alianza kikosi cha kwanza huku nyingine nne akitokea benchi.

 Bao lake la kwanza aliwafunga Coastal Union, bao la pili aliwafunga Namungo FC na bao la tatu aliwafunga Mtibwa Sugar.

Pia mbali na kumpoteza kwa upande wa kucheka na nyavu ameweza kuwa na nidhamu kwa kuwa hana kadi hata moja ya njano tofauti na Luis ambaye ana kadi mbili za njano ile ya kwanza alionyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.
Za Luis hizi hapa:-Mtibwa Sugar dk 90
Biashara United dk 90, Gwambina dk 90.
JKT Tanzania 79, Dodoma Jiji, 79, Prisons 90. Ruvu Shooting dk 90. Mwadui dk 90
Kagera Sugar dakika 90, Yanga dk 90, Polisi Tanzania dk 90, Ihefu 79, Dodoma Jiji 60 na Azam FC 86.
Carlinhos ndani ya ligi:-Mbeya City dk 30, Kagera Sugar dk 35, Mtibwa Sugar dk 72, Coastal Union dk 90 , Namungo FC dk 90, Mtibwa Sugar 29.

 

SOMA NA HII  KUELEKEA 'KARIAKOO DABI'....MIUJIZA YA MWEZI 'APRIL' KUENDELEA KUIBEBA SIMBA MBELE YA YANGA..?