Home Habari za michezo KRAMO AREJEA MSIMBAZI FULUMZUKA CHEKI BALAA LAKE

KRAMO AREJEA MSIMBAZI FULUMZUKA CHEKI BALAA LAKE

Habari za Simba leo

Kiungo mshambuliaji Aubin Kramo amerejea mazoezini baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti aliyokuwa ameyepata mazoezini.

Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema nyota huyo ambaye anasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ndani na nje ya Tanzania, ameanza mazoezi ya pamoja na wenzake wote hapo jana Agosti 29, 2023.

“Kila shabiki wa Simba na mashabiki wote wa mpira Afrika wanatamani kumuona mwamba Aubin Kramo akifanya yake uwanjani, taarifa njema ni kwamba yupo fiti na ameanza mazoezi na wenzake baada ya wachezaji kuingia kambini kumuwinda Power Dynamos,” alisema Ahmed.

Mbali na Kramo, Ahmed alisema beki wao katili Henock Inonga naye amerejea rasmi baada ya kupewa mapumziko ya takriban wiki mbili akiunguza majeraha madogo ya bega.

SOMA NA HII  UONGOZI WA SIMBA AFUNGUKA KUHUSU AJALI YA CHE MALONE ISHU IKO HIVI