Home Habari za michezo GAMONDI: AFUNGUKA KUHUSU WACHEZAJI WAKE KUFUNGA MAGOLI MATANO…. SIO LENGO LETU…AFUNGUKA HAYA

GAMONDI: AFUNGUKA KUHUSU WACHEZAJI WAKE KUFUNGA MAGOLI MATANO…. SIO LENGO LETU…AFUNGUKA HAYA

Habari za Yanga leo

Kocha wa Mkuu Yanga, Miguel Gamondi amesema siyo lengo lake kufunga mabao matano kila mchezo, lakini wachezaji wake wote wana njaa ya kufunga magoli na ndicho wanachokionyesha uwanjani.

Gamondi amesema hayo jana Agosti 29, 2023 mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania na Yanga kufanikiwa kuwafunga maafande hao bao 5-0 ikiwa ni mechi ya tatu mfululizo wakifunga bao 5 kila mechi.

“Mchezo ulikuwa mgumu kidogo kipindi cha kwanza, walijaribu kufanya midblock na kucheza faulo. Tulilazimika kuwa wavumilivu na kutafuta namna ya kuwafungua ili kupata mabao.

“Baada ya kuwafunga bao moja dakika za mwisho za kipindi cha kwanza tulifanikiwa kuwafungua kwa kiasi flani na kipindi cha pili tulicheza mpira mzuri, tulimiliki mpira na kutenegeneza nafasi na kupata mabao.

“Haiwezi kuwa mabao matano kila mechi lakini cha msingi ni kufunga na kushinda kwanza, wachezaji wangu wana njaa ya kufunga mabao, na wanaonyesha uwanjani. Kila mchezaji anaweza kufunga mabao kwenye hii timu sitegemei mchezaji mmoja.

“Ninawapongeza wachezaji wangu kwa kujituma, wamefanya kazi kubwa na nina furaha sana kwa sapoti ninayoipata kutoka kwa mashabiki. Tutajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kufikia malengo yetu. Kwangu ni furaha na bahati kubwa kufanya kazi hapa, staffs wango wote tunafanya kazi kwa kujituma na tuna furaha kwa kila ushindi tunaoupata.

“Ninafurahi pia timu yangu inavyocheza, jambo ninalowaambia kila siku ni timu kwanza wala sio jina la mchezaji, kila mmoja akijituma maan yake timu itacheza vizuri. Konkoni anahitaji muda wa kuizoea Ligi, atafanya vizuri. Tunaye Clement Mzize pia naye anafanya vizuri licha ya umri mdogo,” amesema Gamondi.

FT: YANGA SC 5-0 JKT TANZANIA

45+3’—⚽️ Stephanie Aziz Ki

54’—⚽️ Kennedy Musonda

64’—⚽️ Yao Kouasi

79’—⚽️ Maxi Nzengeli

87’—⚽️ Maxi Nzengeli.

SOMA NA HII  BAADA YA KELELE KUWA NYINGI...SIMBA WAANIKA SABABU ZA KUMPUMZISHA MORRISON...BARBARA AMKAANGA ILE MBAYA...