Home Habari za michezo SIMBA YA ROBERTINHO NI HATARI KILA NAFASI NI BAO

SIMBA YA ROBERTINHO NI HATARI KILA NAFASI NI BAO

Tetesi za Usajili Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC Mbrazili Roberto Oliviera Robertinho ameamua kila faulo itakayopatikana kwa timu yake nje ya 18, inapaswa kuwa bao kwa zaidi ya asilimia 50.

Hiyo ni katika kuhakikisha timu yake inatumia vyema mipira ya kutenga watakayoipata nje ya 18 ya goli la wapinzani wake watakaokutana nao.

Kikosi cha Simba SC juma lililopita kilirejea kambini kujiandaa na mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakaocheza dhidi ya Power Dynamos ya nchini Zambia.

Robertinho amesema anataka kuona vijana wake wanazotumia vyema nafasi za mipira ya adhabu ya faulo wanazozipata nje ya 18 ya goli pinzani mara baada ya Ligi Kuu Bara kuanza wiki mbili zijazo.

Kocha huyo amesema kuwa timu yake imekuwa ikipata mipira mingi ya faulo, ambazo anaamini wangezitumia vyema, basi wangepata ushindi wa mabao katika michezo miwili ya ligi.

Ameongeza kuwa kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju jijini Dar es salaam aliwapa program hiyo ya kupiga faulo akiwatumia nyota wake Clatous Chama, Luis Miqquissone, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’, Hussein Mohammed Tshabalala’ na wengineo.

“Timu yangu bado naendelea kuiboresha lakini mara baada ya kurejea kambini niliwapa program wachezaji wangu jinsi ya kupiga faulo. Hiyo ni baada ya kuona wachezaji wakishindwa kutumia nafasi nyingi za kupiga mipira hiyo ya kutenga nje ya 18,

“Kikubwa ninataka kila nafasi tutakayoipata ya faulo tunaitumia vyema katika kufunga mabao itakayopatikana ya faulo, wapo wachezaji ambao nimewaandaa kwa ajili ya kupiga mipira hiyo,” alisema Robertinho.

SOMA NA HII  FEI TOTO:- KISA KANUNULIWA iPHONE MACHO MATATU ANAMTUSI MAMA YANGU HADHARANI...