Home Uncategorized GWAMBINA FC HALI TETE NDANI YA DAKIKA 360

GWAMBINA FC HALI TETE NDANI YA DAKIKA 360

 


KLABU ya Gwambina FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fulgence Novatus imetumia dakika 360 ndani ya uwanja bila kufunga bao huku ikiruhusu kufungwa jumla ya mabao matano.

Mechi ya kwanza Gwambina FC ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United Uwanja wa Karume kisha mchezo wake wa pili ililazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Gwambina.

Mechi ya tatu Gwambina ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini na mchezo wake wan ne ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Simba, Uwanja wa Mkapa.Ipo nafasi 17 ikiwa na pointi moja.

Jumla imefungwa mabao matano ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 72 ina kibarua kingine Oktoba 3 dhidi ya Ihefu, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nyamagana baada ya ule wa Gwambina Complex kufungiwa na Bodi ya Ligi Tanzania.

 

SOMA NA HII  TANZANIA PRISONS: TUMEWAFUNGA MARA NYINGI SIMBA, TUTAWAFUNGA TENA