Home Habari za michezo FEI TOTO:- KISA KANUNULIWA iPHONE MACHO MATATU ANAMTUSI MAMA YANGU HADHARANI…

FEI TOTO:- KISA KANUNULIWA iPHONE MACHO MATATU ANAMTUSI MAMA YANGU HADHARANI…

Habari za Yanga

Kiungo wa Yanga Feisal Salum katika mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na yeye kutotaka kurudi tena yanga huku akikitaja kitendo cha Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe kumtusi hadharani mama yake kwa kumfananisha na andazi.

Akizungumza kwa uchungu Feisal anasema;

“Kisa kununuliwa macho matatu unakuja hadharani kumtusi mama yangu, yani uitukane pepo yangu halafu nije kukaa na wewe mezani tuzungumze, sio rahisi kwa dharau ulionionesha tunazungumza kitu gani”

Kitendo cha Mchezaji wa Yanga Feisal Salum kukaa pasipo kucheza mpira hata yeye hakipendi kwa kuwa yeye ni mtoto wa Kimasikini na ili apate kipato lazima acheze mpira.

Mbali na hilo Mchezaji huyo amedai mzazi wake ni mgonjwa na yeye ndio anasimamia matibabu hivyo pasipo kupata pesa kupitia kucheza mpira kwake inakua shida.

“Mimi nimetokea kwenye familia ya kimasikini, mimi nasaidia familia yangu, ili mambo yaende ni lazima mimi nifanye kazi, Baba yangu anaumwa na mimi ndio nasimamia matibabu, yeye mwenyewe hapendi hili sakata liendelee kwasababu kuna mambo yanakwama”

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAFUNGUKA MAGUMU HAYA WANAYOPITIA LIGI KUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here