Home Habari za michezo FEI TOTO:- SIJUI KIINGEREZA..WALINISAINISHA MKATABA SIO…GSM ANANIPIGIA SIMU SIPOKEI…

FEI TOTO:- SIJUI KIINGEREZA..WALINISAINISHA MKATABA SIO…GSM ANANIPIGIA SIMU SIPOKEI…

Habari za Yanga SC

Hatimaye Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amefunguka hadharani kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kushinikiza kuvunja mkataba wake na Klabu ya Young Africans mwishoni mwa mwaka 2022.

Fei Toto amefunguka sakata lake na Young Africans alipofanya mahojiano na Clouds FM mapema leo Alhamis (Juni Mosi), ambapo ameseama amepitia kadhia nyingi hadi kufikai maamuzi ya kutaka kuvunjwa kwa mkataba wake.

Kiungo huyo ambaye alionekana kuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Young Africans, hasa katika michezo ambayo ilikuwa mgimu kwa timu hiyo, amesema kwa muda wote alijitoa kuitumikia klabu, lakini manyanyaso yalikuwa machungu kwake na kujikuta akifanya maamuzi ya kujiweka pembeni.

Amesema Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said amekuwa kikwazo kwake mara kadhaa, na mbaya zaidi amekuwa akisema uongo sambamba na kuwaaminisha Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, anapoulizwa sakata linalohusu kuondoka kwake klabuni hapo.

Amesema kiongozi huyo alikuwa akimnyanyasa sana kwa kumtuhumu kuwa anauza mechi na kumwambia kuwa atarudi kwao Pemba, hali ambayo ilipelekea kumwaga machozi hadharani, na pia ikafika wakati injinia Hersi alikuwa hapokei simu yake mbali na kusainishwa mkataba wa miaka mitatu bila kujua.

“Injinia Hersi amenikejeli na ameniudhi sana, nimenyanyaswa sana nikiwa Yanga, nimeambiwa nauza mechi na viongozi.”

“Mara ya mwisho nimekutana na Hersi Mikocheni akaniambia anataka kunirudisha nikamwambia mimi siwezi, akaniambia basi nenda CAS.”

“Kama Rais sio Hersi sasa hivi narudi, sina shida na Yanga akiondoka Rais narudi sina shida na Mashabiki najua wananipenda.” Amesema Feisal

Katika hatua nyingine Feisal Salum akamzungumzia Mdhamini wa Young Africans Ghalib Said Mohamed, kwa kusema naye alimdharau kwa kushindwa kupokea simu zake wakati akitafuta suluhu ya tatizo lake, hivyo anaamini naye alimdharau.

“Pia Ghalib kaniudhi alikua hashiki simu zangu kabla, amenitafuta baada ya kuondoka na mimi sikupokea kwa sababu sipendi dharau hata kama sina kitu”

“Wakati natafuta suluhusho nilimtafuta Ghalib akawa hapokei baada ya kugoma akanitafuta sikumpokelea simu na, Mimi ni maskini lakini hata kama una pesa sitaki dharau.

“Nafsi yangu ilitamani kwenda kuchezea Yanga, nilikubali kwenda kuichezea Yanga kwa kipato kidogo zaidi ya kile ambacho nilikikataa Simba SC, ni kwasababu ya mapenzi tu.

“Yanga ni taasisi kubwa sana, Sina tatizo na Yanga, Sina tatizo na mashabiki wa Yanga nawapenda kama wanavyonipenda najua wameaminishwa vibaya kuwa mimi ni tatizo ndiyo maana niliamua kunyamaza kimya kwasababu najua hawajui kilicho nyuma ya pazia, Mimi nina tatizo na Rais wa timu.

“Nilikutana na Rais wa Timu nikamueleza wazi na alikiri kwa kusema kama amenikosea nimsamehe mimi nikakubali kumsamehe lakini nikamtaka tuyamalize haya mambo kwa kuniruhusu nikatafute maisha kwingine,” amesema Feisal Salum.

SOMA NA HII  KISA JEZI MPYA KUFANANA NA ZA MTIBWA..YANGA WAFUNGUKA HAYA