Home Uncategorized HESABU ZA FOUNTAIN GATE NI NDEFU KWELI

HESABU ZA FOUNTAIN GATE NI NDEFU KWELI


 UONGOZI wa timu ya Fountain Gate umeweka bayana kuwa maisha yao ndani ya Ligi Daraja la Kwanza hayatakuwa marefu kwa kuwa mpango wao namba moja ni kushiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa timu hiyo iliyo kundi B na pointi zake 10 baada ya kucheza mechi nne, Juma Ayo alisema kuwa hesabu kubwa ni kuona timu inashiriki Ligi Kuu Bara jambo litakalowapa tabasamu wachezaji pamoja na viongozi.

“Kwa sasa mambo bado hayajaeleweka ili kila kitu kiwe sawa ni lazima tuone timu inapanda Ligi Kuu Bara hapo ndipo furaha yetu kubwa itaonekana ndio maana kwa sasa tunapambana kwa hali na mali kupata ushindi kwenye mechi zetu.

“Ushindani ni mkubwa nasi pia tunashindana kwani ugumu wa mapambano unatufanya nasi tuongeze juhudi kuanzia maandalizi na kwenye mchezo wenyewe, mashabiki watupe sapoti,” alisema Ayo.

 

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA ANGA ZA UD SONGO, KULIVUTA JEMBE HILI LA KAZI