Home Yanga SC INJINIA HERSI AKIRI MAMBO MAGUMU YANGA

INJINIA HERSI AKIRI MAMBO MAGUMU YANGA


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga mhandisi Hersi Said amesema hatua ya timu yao kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union ni muendelezo wa kutopata matokeo mazuri katika Uwanja wa CCM Mkwakwani.

Yanga imepoteza mechi yake ya kwanza msimu huu katika Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union kwa mabao 2-1 matokeo ambayo yamesitisha safari yao ya kutofungwa.

Hersi amesema matokeo hayo yanawapa elimu kwamba wanatakiwa kujitathimini ni wapi wanakosea kila wanapofika katika Uwanja huo kwa mwaka wa tano sasa bila kupata ushindi.

“Haya matokeo sio mazuri kwetu lakini yanatupa nafasi ya kufahamu kwamba Uwanja wa Mkwakwani ni mgumu kwetu tunapoteza kwa miaka mingi sasa,” amesema Hersi.

“Kila Mwanayanga anatakiwa kutumia nafasi yake kutafakari ni wapi tunakosea kila tunapokuja sasa mkoani hapa, ilikuwa hivi pale Jamhuri Morogoro na tukabadilisha mambo msimu huu tuumize kichwa sasa na Mkwakwani.

Aidha Hersi amesema matokeo hayo pia yanatakiwa kufanyiwa tathimini kwa wachezaji wao ambapo watakutana nao mara baada ya kufika Arusha.

” Sio afya kuongea na wachezaji sasa baada ya matokeo haya lakini tutaongea nao tukifika Arusha kusikia wanakipi kilituangusha.”

SOMA NA HII  FISTON AAHIDI MVUA YA MABAO, UBINGWA YANGA