Home video GOMES:LAZIMA TUWE TAYARI,AWACHAMBUA WACHEZAJI WAKE

GOMES:LAZIMA TUWE TAYARI,AWACHAMBUA WACHEZAJI WAKE

DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana unaotarajiwa kuchezwa nchini Botswana, Oktoba 17 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Oktoba 22.


 Gomes ameweka wazi kuwa ishu kubwa ambayo inawatesa kwa sasa ni suala la wachezaji wake kuwa majeruhi ikiwa ni pamoja na Sakho ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hivyo bado hajawa tayari.

 Licha ya yote hayo Gomes amesema kuwa ni lazima wawe tayari kwa aili ya kupambana na anaamini kwamba mchezo huo hautakuwa mwepesi lazima utakuwa mgumu kwa namna yoyote ile ila kazi yao ni kuweza kusaka matokeo.

 

SOMA NA HII  VIDEO: TFF YAFUNGUKIA KUHUSU NAMNA WANAVYOFUATILIA KWA UKARIBU KUHUSU MDAMU