Home Habari za michezo AHAMED ALLY AJA NA JIPYA KUHUSU KRAMO, ISHU IKO HIVI

AHAMED ALLY AJA NA JIPYA KUHUSU KRAMO, ISHU IKO HIVI

Habari za Simba leo

Nyota mpya wa Simba SC, Aubin Kramo yupo nchini na hajaenda kutibiwa nchini kwao kama ilivyoripotiwa awali.

Akizungumzia hali yake, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema Kramo anaendelea na matibabu nchini.

“Aanaendelea na matibabu na kumekuwa na taarifa nyingi ooh ameruhusiwa kwenda kwao, Kramo yupo nchini anaendelea kutibiwa na madaktari wa Simba SC,” alisema Ahmed Ally.

Kramo aliyesajiliwa dirisha kubwa lililopita, ameandamwa na majeraha na hajapata muda wa kucheza mechi yoyote ya kimashindano katika msimu mpya ulioanza.

SOMA NA HII  SAMATTA AWATAMBIA WA NIGER KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA